Njia rahisi zaidi kwa wanamuziki kufikisha muziki kwenye Spotify.
Ufikiaji wa papo hapo kwa
Instant
Spotify for Artists
Wanamuziki, jiungeni sasa!
Wasanii 1,000,000+ wanategemea DistroKid. Jisajili hapa.

Barua pepe tayari imesajiliwa (tafadhali ingia)
Ulimaanisha:
Manenosiri hayo yanatofautiana
Tafadhali chagua nenosiri refu zaidi
Tafadhali chagua nenosiri refu zaidi

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
(na majibu!)

DistroKid ni nini?

DistroKid ni huduma kwa wanamuziki inayouweka muziki wako kwenye maduka ya mtandaoni na majukwaa ya utiririshaji. Kisha watu wanaposikiliza muziki wako, tunakutumia pesa.

Kwanini nitumie DistroKid?

Muziki wako wote unapaswa kuwa madukani. DistroKid ndiyo huduma pekee inayokuwezesha kupakia bila ukomo muziki madukani kwa bei moja ya chini. Majukwa mengine hukulipisha kila wakati unapakia kitu—hiyo haifurahishi sana (na kwa gharama ya juu zaidi.

Pia, DistroKid hufikisha muziki wako madukani haraka sana ikilinganishwa na muda ambao washindani wetu hutumia kuweka muziki wako madukani. Tuna huduma bora kwa wateja, takwimu za kila siku, na kiolesura rahisi, pia.

Nani hutumia DistroKid?

DistroKid ni kwa ajili ya wanamuziki wanaofanya kazi peke yao, bendi, ma DJ, watumbuizaji, watayarishaji wa muziki na watengeneza maudhui wa YouTube wanaorekodi muziki wao nyumbani au studio. Vilevile tuna huduma kwa ajili ya lebo.

Itanigharimu kiasi gani?

$22.99 pekee kupakia bila ukomo ya nyimbo na albamu kwa mwaka.

Je, DistroKid huchukua kiasi gani cha mauzo yangu?

Hakuna. Unabaki na 100% ya mrabaha wako.

Upendo wa DistroKid

Mwanamuziki Arizona Zervas

"DistroKid imekuwa jukwaa bora la kutolea muziki wangu kwa miaka mingi!"

- Arizona Zervas

Jarida la Billboard liliandika kwamba Arizona alikuwa 'Msanii wa kwanza kwa Miaka kadhaa kuongoza kwenye Spotify bila Usaidizi wa Lebo' wakati wimbo wake, 'Roxanne', ulipofika Namba 1 kwenye chati ya nyimbo 50 bora za Spotify nchini Marekani.

Wanamuziki Kei Henderson na 21 Savage

"Ninaipenda DistroKid kwa sababu ni rahisi sana kutumia na hakuna mtu wa kati."

- Kei Henderson, 21 Savage

Kei anamsimamia msanii wa DistroKid 21 Savage. Awali, Kei alimsimamia Key!, ambaye kwa sasa amesainiwa na kundi la A$AP Rocky, liitwalo AWGE. Kabla ya hapo, Kei alimsimamia Siya, ambaye alishirikishwa katika mchezo wa TV uitwao 'Sisterhood of Hip Hop' kutoka kituo cha Televisheni cha Oxygen.

Mwanamuziki Megan Davies

"...ni msambazaji bora zaidi wa kidijitali sokoni."

- Megan Davies

Megan ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Nashville. Wakati wa majira ya joto ya 2013, Megan alianza kupakia kava za nyimbo alizotengeneza kwa ala za vyombo visivyotumia umeme kama vile gitaa pamoja na kufanya mashups. Tangu wakati huo, mitindo yake bunifu imemletea wafuasi milioni 1.5 kwenye YouTube na zaidi ya wasikilizaji milioni 2 kila mwezi kwenye majukwaa makuu ya kutiririsha muziki. Megan amekuwa na DistroKid tangu alipoachia wimbo kwa mara ya kwanza.

Mwanamuziki Dan the Automator

"DistroKid ni rahisi, yenye ufanisi, na inafanya kazi!"

- Dan the Automator

Dan 'The Automator' Nakamura ni mtayarishaji wa muziki wa hip-hop mwenye makazi yake San Francisco ambaye kazi yake na 'Kool' Keith Thornton kwenye mradi wa Dr. Octagon ilimletea umaarufu usiotarajiwa mwaka 1996. Kupitia mfululizo wa miradi dhanifu kadhaa iliyochanganuliwa kwa kina tangu wakati huo, utayarishaji wa Nakamura uliojaa ubunifu wa hali ya juu na ucheshi wake wa kipekee vilimfanya awe mmoja wa watu muhimu walioongoza harakati za chinichini za kufufua muziki wa rap mbadala mwishoni mwa miaka ya 1990. Dan ni miongoni mwa wanaounda kundi la Deltron 3030, Dr. Octagon, Handsome Boy Modeling School, Got a Girl, Lovage, Gorillaz, na wengine .

Mwanamuziki Ari Herstand

"DistroKid, inazidi majukwaa mengine kwa mbali, na kwa hakika ndio njia rahisi na ya haraka zaidi ya kufikisha muziki kwa watu weng."

- Ari Herstand

Ari Herstand ametokea kwenye chati ya nyimbo 10 bora kwenye iTunes, akatumbuiza pale Ellen na nyimbo zake nyingi zimetumiwa katika filamu, michezo ya televisheni na matangazo ya kibiashara. Yeye ndiye mwandishi wa How To Make It in the New Music Business, mwandishi mwajiriwa wa Digital Music News na mtengenezaji wa blogu ya ushauri wa biashara ya muziki, Ari's Take.

Mwanamuziki Dweezil Zappa

"Ni rahisi sana kutumia na ina mtindo bora wa kibiashara unaomjali kwanza msanii."

- Dweezil Zappa

Dweezil Zappa ni mpiga gitaa wa muziki wa rock kutoka Marekani. Yeye hurekodi na kutumbuiza peke yake, yaani msanii solo, na pia akiwa na vikundi mbali mbali vikiwemo Zappa Plays Zappa—ambayo ni heshima kwa baba yake, Frank Zappa. Dweezil ametumbuiza na kurekodi na Herbie Hancock, Stevie Ray Vaughan, Bonnie Raitt, Terry Bozzio, The Fat Boys, Nuno Bettencourt, Gary Cherone, Zakk Wylde, na wengine wengi.

Mwanamuziki Ludacris

"DistroKid ndio mambo yote."

- Ludacris

Ludacris ni mmoja wa marapa waliofanya vizuri zaidi kimauzo katika historia ya muziki huo. Ameshinda tuzo za Grammy, Screen Actors Guild, Critic's Choice, na MTV. Mwaka 2017, Ludacris alichagua DistroKid kuachia wimbo wake, 'Vitamin D (akimshirikisha Ty Dolla $ign)'.

Mwanamuziki Rob Scallon

"Tangu mwanzo nimekuwa nikifanya juhudi kubwa kuipendekeza [DistroKid] kwa wanamuziki wengine tangu wakati huo."

- Rob Scallon

Rob ni mchezaji wa vyombo mbalimbali vya muziki, msanii anayerekodi, na mtayarishaji wa muziki. Kwenye YouTube, kazi za Rob zimetazamwa kwa mamilioni, na pia ana wafuasi karibu milioni moja wanaomfuatilia. Kama Guitar World walivyoandika, Rob ni 'mpiga gitaa wa mtandaoni—na pengine ni kitu cha karibu zaidi kwa mtu anayekaribia kuwa shujaa wa gitaa katika kizazi tata tunachoishi siku hizi.'

Mwanamuziki Buck Nasty

"Sioni kampuni yoyote iliyo bora kuizidi Distrokid. Nadhani huu utakuwa ni uhusiano wa milele."

- Buck Nasty

Buck Nasty ni mtayarishaji wa muziki mwenye mauzo ya kiwango cha Platinum kupitia nyimbo 'Hit The Quan' na 'Lean & Dabb' zilizoimbwa na iHeartMemphis (zote zimesambazwa na DistroKid), na nyingine nyingi.

Mwanamuziki Emma Lee

"Ninapenda kwamba unaweza kupakia nyimbo bila kikomo kila mwaka. Kipengele ninachokipenda zaidi ni cha kuwezesha kugawanya mapato."

- Emma Lee

Emma-Lee kutoka Toronto, Ontario, Kanada ni mshindi wa tuzo, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za pop aliyejizolea umaarufu mkubwa. Nyimbo za Emma-Lee zimetumika katika filamu na michezo mingi ya televisheni. Wimbo wake wa karibuni kabisa, 'Worst Enemy', ulikuwa katika nyimbo bora 20 za Billboard nchini Kanada mwaka 2016.

Mwanamuziki Propagandhi

"Tunatumia DistroKid kufikisha muziki wetu kwa maelfu ya huduma za usambazaji za kidijitali zinazoendelea kupanuka kwa haraka na kwa ufanisi zaidi ."

- Propagandhi

Propagandhi ni bendi kongwe ya muziki wa punk ambayo imetoa rekodi nyingi katika historia yao ya miaka 25+.

Mwanamuziki John LaMacchia

"Vitu viwili ninavyopenda zaidi kuhusu DistroKid ni urahisi wake, na bei yake ya chini."

- John LaMacchia

John hupiga gitaa kwa bendi kongwe ya muziki wa hardcore/metal, Candiria. Pia hupiga na Spylacopa, na pia anaendesha lebo inayojitgemea ya kurekodi iitwayo Rising Pulse Records.

Mwanamuziki Zach Marsh

"Ninaipenda DistroKid kwa sababu mimi hutoa kiasi kikubwa cha kazi ya sanaa mtandaoni na DistroKid haina kikomo."

- Zach Marsh

Zach Marsh ni mtunzi kwa ajili ya filamu na michezo ya TV huku akiwa ameandika 'Daredevil' na 'Veggie Tales' za Netflix. Zach pia anaendesha kituo cha YouTube kinachoitwa PiaknowItAl kinachotoa mafunzo ya piano.

Mwanamuziki Ryan 'Fluff' Bruce

"DistroKid ilikuwa nami wakati nikianza na imekua pamoja nami muda wote huo! Endapo DistroKid ingekuwa chakula, basi ingekuwa nyama."

- Ryan 'Fluff' Bruce

Mhandisi mtaalamu wa sauti, mtayarishaji na mtunzi wa nyimbo. Chaneli maarufu ya YouTube ya Ryan inayoitwa 'Riffs, Beards & Gear', ina wafuasi zaidi ya 385,000.

Mwanamuziki Todd Bryanton

"DistroKid ndiyo njia ya haraka zaidi na ya kuaminika kwa kusambaza muziki wangu."

- Todd Bryanton

Todd Bryanton ni mtunzi wa filamu na TV, na pia ni Mwana YouTube ambaye hutoa muziki wa kielektroniki kwa jina LilDeuceDeuce. Video za muziki kwenye kituo chake cha LilDeuceDeuce zimetazamwa zaidi ya milioni 32.

Mwanamuziki Christopher Tin

"DistroKid imekuwa yenye usaidizi mkubwa kwa yale mahitaji ya dharura ya usambazaji."

- Christopher Tin

Christopher Tin ni mtunzi aliyeshinda tuzo za Grammy mara mbili, na ndiye mtunzi wa kwanza kuwahi kushinda tuzo ya Grammy ya muziki kutoka kwenye mchezo wa video.

Mwanamuziki Anthony Vincent

"DistroKid ni rahisi kutumia, yenye ufanisi, na ina ukamilishaji wa haraka sana. Nina furaha sana."

- Anthony Vincent

Anthony Vincent ana zaidi ya wafuasi milioni 2 kwenye Kituo chake cha YouTube, Ten Second Songs—ambapo huzalisha mashups za nyimbo maarufu kwa mitindo mbalimbali ya wasanii wa muziki.

Mwanamuziki Sebstian Olzanski

"Mimi hutumia Distrokid kwa kila wimbo ninaoutoa. Ni tovuti ya haraka na rahisi kuitumia ambayo husambaza wimbo au albamu yoyote ulimwenguni kote!"

- Sebastian Olzanski

Sebastian Olzanski ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo mwenye umri wa miaka 17. Sebastian ana wafuasi zaidi ya milioni 1 kwenye mitandao yake ya kijamii.

Mwanamuziki Saher Galt

"Ninautoa muziki wote ninaotaka kwa ada moja ya chini. Hakuna vizuizi kati yangu na kuupeleka muziki wangu ulimwenguni. Swadakta."

- Saher Galt

Saher Galt ni mwimbaji, mtunzi, na mwanzilishi-mwenza wa Galt Aureus, kundi la wanamuziki wawili wa muziki wa rock wenye tuzo. Saher pia hutoa mafunzo ya kutayarisha muziki na mafunzo ya kuimba kwenye kituo chake cha YouTube, ambacho huwafikia mamilioni ya watazamaji.

Mwanamuziki Joel 'Roomie' Berghult

"DistroKid imerahisisha na kwa kweli imeleta mapinduzi ya usambazaji wa kidijitali."

- Joel 'Roomie' Berghult

Joel 'Roomie' Berghult ni msanii anayejitegemea ambaye kufikia Novemba 2016 alikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 2.5 kwenye mitandao yake ya kijamii. Anajulikana kwa uwezo wake wa kuimba kwa sauti tofauti tofauti na mara nyingi hushirikiana kutoa muziki na Pewdiepie, mtu anayefuatiliwa zaidi ulimwenguni kwenye mitandao ya kijamii.

Mwanamuziki Claire Wilkinson

"DistroKid ndie msambazaji wa haraka zaidi na mwenye ufanisi anaepatikana sokoni."

- Claire Wilkinson

Claire Rachel Wilkinson, anayejulikana kama Clairity, ni mwimbaji-mtunzi wa nyimbo mwenye umri wa miaka 19. Kava aliyoimba Clairity iitwayo 'Don't Panic' ya Coldplay ilitokea kwenye tangazo la filamu ya 'X-MEN: Apocalypse' kutoka 20th Century Fox.

Mwanamuziki Glenn Fricker

"DistroKid ni nzuri katika kuondoa vikwazo vya kuweka muziki wangu mtandaoni. Ninapakia sehemu moja na kukusanya mapato yangu."

- Glenn Fricker

Glenn Fricker ni mhandisi, mwendeshaji wa chaneli ya YouTube, na mmiliki wa SpectreSoundStudios. Kwenye YouTube, kazi za Glenn zimetazamwa takribani mara milioni 100 na wafuasi 435,000 wanaoifuatilia . Glenn, anayejulikana kama 'mtu mwenye hasira zaidi nchini Kanada,' anatambulika kwa kuwa ni msema ukweli (kitu ambacho huwakasirisha baadhi ya wazalishaji).

Mwanamuziki Ray Harmony

"Siku niliyoigundua DistroKid ilikuwa ni mojawapo ya siku za furaha zaidi katika miaka yangu 20 ya kazi ya muziki! Hatimaye, kulikuwa na kampuni ya usambazaji ambayo iliwaelewa wanamuziki."

- Ray Harmony

Ray Harmony amejitolea maisha yake kutumia ushawishi wa muziki kuhamasisha mabadiliko chanya ulimwenguni, ambayo hufanya kupitia Revolution Harmony. Yeye ni mhadhiri wa muziki ambae ni mshindi wa tuzo, mtunzi, mwigizaji, mtayarishaji wa muziki, mwanahabari, na mwandishi. Ray pia hutengeneza muziki na washindi wa tuzo za Grammy za platinamu kadhaa (Serj Tankian wa System of a Down, Tom Morello wa Rage Against the Machine, na wengine wengi)—kisha hutoa mapato yote kwenye mifuko ya hisani.